‘Mimi sio store ya magonjwa!’ Rose Muhando awaambia waliosema amelazwa hospitalini

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando ameamua kuwazima wambeya ambao wamekuwa wakimuelezea kama mtu aliyelaaniwa ama mgonjwa ambaye anatakiwa kutubu.

Msanii huyo ambaye aliwahi kuvuma sana alikerwa sana na uvumi uliokuwa ukienezwa kuwa amelazwa hospitalini tena miezi chache baada ya kuondolewa.

Akizungumzia jambo hilo kwenye mitandao yake ya kijamii ya youtube, Rose alikuwa na haya ya kusema,

"LEO HII KUNA CLIP INATEMBEA MITANDAONI ROSE MUHANDO ANAUMWA SANA AMELAZWA HOSPITALINI…UKWELI WAPENDWA NAUMIA SANA KILA MARA KUTAMKIWA MAGONJWA. MIMI SIO STORE YA MAGONJWA. WASIFIKIRI KUWA SHETANI ANA NYUMBANI KWAO. SIDHANI KWAMBA WAO WAKO SALAMA SANA MPAKA WAONE MAGONJWA HAYO YALILETWA KWA SABABU YANGU." Alizungumza.

Alizidi na kukana madai haya na huu hapa usemi wake wa mwisho kuhusiana na uvumi huo.

"DO NOT GIVE THE CHURCH WORK OF PRAYER AND FASTING FOR NO REASON. I AM WELL AND HEALTHY. I AM WORKING FOR GOD. I GOT THE NEWS WHEN I WAS REHEARSING FOR MY NEW ALBUM AND I DECIDED TO ADDRESS THIS. I’M NOT SICK."

Rose alimshtumu mwanamume aliyefahamika kama Silas kwa kueneza uvumi huo, hizi hapa hisia za mashabiki wake kuhusiana na tendo hilo.

Sarah Irara Wachaneni na Rose asifu Mungu wake, Mungu amlimpa uponyaji amtumikie. Lord silence every evil tongue against your servant 🙏🙏🙏

Blessed Mum Happy to see you mum,nilikuwa nimeshangaa kuona hiyo clip.

Knew Tech Live long life mommy. Hupigani mwenyewe unapiganiwa na mungu!huyo Silas ashindwe na alegee kwa jina layesu

Furahini Mbwambo Waache waseme ili Mungu awalipe vizuri, Kama wema ni akiba na ubaya pia ni akiba , Rose piga injili mpaka shetani achanganikiwe

Dives Thank God it was not true mama yao

Juliana Kilo Wakenya tunakupendaaaa, God is with you

Nelly Liz Usiogope naneno yao usitetemeke mbele yao usifadhaike mbele yao Rose sheitani isikusumbue anyamaze kimia na akatoweke Kara jina la Yesu Rose umeshinda tena zaidi ya kushinda

Anastacia Muchina Washidwe kwa jina la yesu mwimbie mungu rose ndio wachanganyikiwe.