Miungu ya bahari ilitaka damu ya Mariam na Amanda, familia yatoa tamko

fer_0
fer_0
Tukio la Mariam Kaghenda na mtoto wake Amanda Mutheu limetokea na taarifa kwamba huenda bahari ikawa na 'wenyewe.'

Mama huyu na mtoto wake walizama katika kivukio cha Likoni yapita sike saba.

Oguna ametangaza kuwa kikosi cha wanamaji na wapiga mbizi kutoka Afrika Kusini kinatarajiwa nchini.

Kikosi hiki kitasaidia katika juhudi za operesheni Bahari ya Hindi kivukio cha Likoni.

Katika taarifa kwa wanahabari, Cyrus Oguna amesema kuwa serikali imetafuta msaada wa wapiga mbizi kutoka Afrika kusini ili kusaidia kutoa gari la Mariam Kigenda na mtoto wake wa miaka 4 Amanda Mutheu.

Ila je? Huenda miungu wa baharini wana mchango mkubwa kwa juhudi hizi kugonga mwamba?

Wazee wa mijikenda sasa wanahoji kuwa miungu ya bahari imekasirika kwa muda mrefu na ni wakati wa kuipa kupitia kafara ya damu.

Kauli ambayo inazungumziwa sana na wenyeji wa pwani imepata maoni kinzani katika mitandao ya kijamii.

Wengi wapo na nia kuwa kuchinjwa kwa mnyama na kisha damu yake kumwagwa kwenye eneo la tukio ili kusababisha miili ya waathiriwa kujitokeza itakuwa ya msaada mkubwa zaidi.

"Zamani , mtu alipopotea,watu walikusanyika na kutafuta ng'ombe mweusi mwenye paji nyeupe, wakamchinja katika eneo alilozama kisha wakamwaga damu kwenye bahari... " Alihoji mwenyeji.

Wanakijiji na wakaazi wanahoji kuwa miungu ya bahari ina njaa kwa muda mrefu kwa hivo walitaka damu yua Mariam na Mutheu kama kafara.

Familia ya Mariam imejitenga na taarifa za miungu na kusema kuwa hawatachinja ama kumwaga damu.

"Hatuamini katika itikadi kama hizo zinazopingana na ukristo wetu..."

"Tutazidi kuomba na watu wetu watapatikana katika jina la Yesu kristo..." Alisema msemaji wa familia Luke Mbati.