Mkasa wa Feri, Bassen aomba wakenya radhi, apanga kusafiri nyumbani

unnamed (1)
unnamed (1)
Volker Bassen hatimaye amekiri kuwa sio rahisi kufikia gari na miili ya Mariam Khagenda, 35  na Mutheu kama alivyodhania.

Matumaini ya kupata gari na miili inadidimia kila uchao baada ya taarifa za hali ya hatari Bahari Hindi.

Kina cha Bahari Hindi kina urefu mkubwa zaidi ambao ni kisiki cha kuendesha zoezi hilo.

Ni kwa urefu huu ambapo Cyrus Oguna anapendekeza kutumia roboti kupiga picha na kukusanya data ya hali ilivyo majini.

Soma hadithi nyingine:

Majini kuna samaki aina ya Papa ambao ni hatari kwa usalama wa binadamu yeyote.

Mswidi Volker Bassen amekata tamaa na kutangaza kurudi nyumbani kwao leo Jumamosi.

Bassen amesema kuwa uwezo wa kuona chini ya Bahari Hindi ni muhali mno.

Bassen ameomba radhi wakenya wamsamehe kwa kuwa awali alikuwa ametangaza zoezi hilo atalifanya kwa masaa mawili.

Soma hadithi nyingine:

Mswidi huyu amesema kuwa ni vigumu na tena kuhatarisha maisha kwa sababu ya giza kubwa chini ya bahari.

“Ningependa kufuta kauli yangu ya awali kuwa ningeipata gari hiyo na miili kwa muda wa masaa mawili...' Aliomba radhi Bassen.

Ndugu na familia ya Mariam wanaeleza matumaini waliyokuwa nayo kwa mpiga mbizi huyu,

Soma hadithi nyingine:

“Tulihisi uchangamfu mwingi na matumaini makubwa baada ya kuona wapiga mbizi wengi wamekuja kuokoa..."

Bassen amenukuliwa kwamba yeyote anaingia mle lazima awe na ngao ya kumkinga na papa hawa.

Amesema kuwa wapiga mbizi wanahatarisha maisha yao kuogelea bila kinga imara.

Gari na miili ya marehemu inakisiwa kuwa Mita 100 kwenda chini ya bahari, katika sehemu kama hii kuna kiza kinene ambacho hakimruhusu mpiga mbizi kuona kwa urahisi hivyo kumbidi awe na chombo cha kutoa mwangaza.