Mkewe Bahati , Diana Marua afunguka maisha ya ulevi

Screenshot_from_2019_12_20_16_26_21__1576848403_98685
Screenshot_from_2019_12_20_16_26_21__1576848403_98685
Mkewe Bahati Diana Marua amefunguka kuhusu tofauti ya maisha yanayozingira uraibu wa kwenda densi klabu na ndoa.

Akiwajibu baadhi ya mashabiki waliohoji kuwa bado anayakosa sana maisha ya klabu na kujiburudisha, Marua amesema kuwa alishachoka na maisha hayo na kuwa sasa anachokizingatia zidi ni maisha ya ndoa.

https://www.instagram.com/p/B6NUaLIgrkv/

“Hebu niwaambie kuwa hayo yote nishafanya. Nilifanya yote hayo. Hiyo parte after parte nishachoka. Yaani I served my life a good one mpaka sahii mimi hukaa chini nauliza leo ni Friday watu wako dunda? Watu wako tu huko wanashake their bum bum and doing other stuff. Sina muda huo, kwa sasa mimi ni mama wa watoto watatu na nishatulia. Nadhani nishafanya hayo yote na niko poa na jinsi nilivyo sasa...' Alisema Diana.

Haya yanajiri baada ya kufunguka kuwa kabla ampate Bahati, aliishi maisha ya ulevi na kwenda klabu.

Kulingana na Diana, Bahati alimvuta na kumleta kwa Mungu na hapo akaacha ulevi.

“Niliheshimu sana Bahati sana na nikijua kuwa naenda kumwona Bahati, ningetafuna PKs nyingi kuficha harufu ya pombe. Alikuwa anajua tu nimelewa kidogo japo nilijitahidi kuiyeyusha hali...' Alisema Marua katika mahojiano ya awali.