Mkurungenzi mkuu wa NYS afikishwa hospitalini baaya ya kunywa chai

Mkurugenzi mkuu wa NYS Matilda Sakwa alipelekwa hospitalini baada ya kunywa chai akiwa ofisini mwake siku ya jumanne.

Kulingana na msemaji wa NYS, inashukiwa kuwa chai aliyokunywa ndio iliyomsababishia matatizo hayo mwilini mwake.

Inasemeka kuwa huenda kuna mtu aliyetaka kumuangamiza Sakwa.

Sakwa amekuwa kwenye harakati za kulisafisha jina la NYS lililokuwa limekumbwa na visa viwili vikubwa vya ufisadi ndani ya miaka miwili. Kisa cha kwanza kilihusisha kima cha shillingi billioni saba huku cha pili kikihusisha kima cha shillingi billioni mbili.

Kulingana naye Sakwa, ufisadi ni janga kuu kwa taifa kama Kenya huku pia akijua kupigana na ufisadi ni jambo nzito sana. Sakwa alisema,

" Najua kupigana na Ufisadi huchukua muda ila najitahidi kulisafisha jina la NYS na nipo tayari kupatana na changamoto kama hizi."

Baada ya kupewa kazi ya NYS, Sakwa alianza kwa kuleta madaraka yote ya fedha kwenye kituo kikuu ili kusaidia kupunguza ufisadi."

"Tuliona kuwa jambo njema lilikuwa ni kuleta bajeti zote pamoja kisha pesa za idara zote 22 zitatoka kwenye ofisi kuu ya NYS ilikusadia kupunguza ufisadi," Sakwa alieleza gazeti la the star baada ya kutoka hospitalini.

Sakwa alieleza kuwa bajeti za NYS sasa zinatolewa kulingana na idadi ya wanafunzi walioko katika vituo husika.

Mfano,Nairobi iliyo na wanafunzi elfu kumi na nne itapata kima cha millioni mia nne huku imbalambala iliyo na wanafunzi elfu mbili ikipata kima cha milioni nne.