Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Tarehe 12 Juni 2019

  

 Korti yazidisha muda wa kuzuia wabunge kulipwa marupurupu ya nyumba

  WABUNGE  wamepata pigo  baada ya mahakama kuzidisha muda wa agizo la kuwazuia  kupokea marupurupu ya nyumba ya shilimngi elfu 250 kila mwezi . SRC ilikuwa imewasilisha kesi  ikitaka wabunge kuzirejesha fedha hizo walizokuwa wamelipwa  ikisema hatua hiyo ni ukiukaji wa sheria . agizo hilo litaendelea kutekelezwa hadi juni tarehe 24 wakati  kesi hiyo itakaposikizwa .

  Mtoto aliyeibwa Naivasha afariki

  Mtoto mchanga anayeshukiwa kuibwa na mwanammke mmoja huko naivasha ameaga dunia baada ya kupata matatizo ya kupumua . naibu OCPD  wa naivasha  JoHN Kwasa  AMESEMA mwanamke aliyekuwa amemwiba mtoto huyo anahojiwa na polisi .

 Maafisa 10 wa KDF katika ajali ya barabarani .

 Maafisa kumi wa KDF  wanapokea matibabu katika hospitali ya Forces memorial  baada ya kujeruhiwa katika ajali  ya barabarani katika eneo la mutindwa kwenye barabara ya kangundo mapema leo . kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya matungulu ISAAC thuranira  amesema dreva  wa lori hilo  lililokuwa limewabeba maafisa 18 wa KDF  alishindwa kulithibiti na kulifanya  kulisababisha kuanguka

  Mvua kutawala Kisumu,Siaya na Homabay

  Kaunti za Kisumu, Siaya, Homabay, Kericho  na  Nakuru c ni baadhi ya zinazotarajiwa kushuhudia mvua kubwa katika siku tano zijazo . idara ya utabiri wa hali ya anga  imesema hali ya kibaridi na mawingu itatawala sehemu za  Nairobi, Nyandarua, Laikipia, Nyeri, Meru, Embu na  Tharaka  Nithi .

Wachina wanaofanya biashara ndogo ndogo kurejeshwa  nchini mwao-Matiang'i

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi  ameaigiza kurejeshwa nchini mwao raia wa Uchina  wanaofanya biashara  katika soko la Gikomba  hapa jijini . Matiangi amesema wachina hao wapo nchini kinyume cha sheria . Matiangi amesema raia wote wa kigeni wanaoshiriki biashara ndogo ndogo nchini watarejeshwa makwao.

 Mtoto aliyeambukizwa  ebola Uganda afariki

Mtoto mwenye umri wa miaka mitano  nchini Uganda   aliyepatikana na virusi vya Ebola ameaga dunia .shirika la afya duniani WHO limesema  kisa hicho kilikuwa cha  kwanza kilichothibitishwa nchini humo baada ya kuchipuka kwa ugonjwa huo katika taifa la DRC  .

 Mwalimu auawa ,Polisi 2 wajeruhiwa katika shambulzi la majangili Turkana

Mwalimu  mmoja wa shule ya msingi  ameuawa kwa kupigwa risasi ilhali maafisa wawili wa polisi wa utawala  wamejeruhiwa baada ya gari la polisi kushambuliwa na majangili  huko Turkana mashariki .kamanda wa polisi wa kautni ya Turkana  Samuel Ndanyi  amesema gari hilo la polisi lilikuwa likielekea katika kituo cha kibiashara cha  Lokori kutoka Napeiton .

  Mwanamme amwua mkewe Matayos

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 25 ametorokea mafichoni baada ya kumuua mkewe kwa kumudunga kisu katika  eneo la Khujibi , Matayos kaunti ya Busia. Jamaa huyo anadaiwa kuanza  kumpiga mkewe wakati wa usiku kabla ya  majirani kuingilia kati ingawa mkewe alifariki baadaye kutokana na majeraha ya visu.

 Nakuru sasa ni kituo cha huduma za paspoti

   Iwapo unaishi nakuru  au maeneo yanayopakana na mji huo basi una cha kukupa tabamasamu kwani hutalazimika kupiga kambi katika jumba la nyayo hapa Nairobi kupata paspoti au kubadilisha  iliyojaa . waziri wa usalama wa ndani Fred matiangi  amesema tangu septemba mwaka  wa 2017  takriban  watu milioni moja wamepata paspoti mpya au kuchukua za kisasa .

  FBI kuisadia Kenya kupambana na ufisadi

  Shirika la uchunguzi nchini marekani FBI  liemeahidi kuisaidia Kenya katika vita dhidi ya ufisadi .hii ni baada ya mkutano kati ya   mkuu wa dci George kinoti ,mkurugenzi mkuu w amashaka ya umma Noordin Haji na naibu mkurugenzi wa FBI  David Bowdich . kundi hilo lipo katika ziara ya siku tatu nchini marekani .

 City hall yatangaza wazi nafasi  za maafisa wakuu

 City Hall  imetangaza wazi nafasi kumi za wakuu wa idara ,mkurugenzi wa zabuni na katibu wa jiji .hii  ni baada ya ufichuzi kwamba  kandarasi za baadhi ya maafisa wakuu wa CITY hall zilitamatika  mwezi aprili .una hadi  tarehe 24 kutuma maombi ya kazi hizo .

  Bunge la  Murang’a lapitisha bajeti yake  ya 2019/2020

Bunge la kaunti ya murang’a limeidhinisha bajeti ya  shilingi bilioni 8.9 ya mwaka wa 2019/2020. Mwenyekiti wa kamati ya bajeti  Kibe Wasare  amesema baadhi ya idara zilizonufaika pakubwa na bajeti hiyo ni  afya ,kilimo ,kawi ,elimu na miundo msingi .