Mgane wa marehemu gavana wa Bomet Joyce Laboso, ameteuliwa kuwa mwanachama wa kamati ya ushauri kuhusu mashirika ya serikali .katika uteuzi uliotangazwa na rais Uhuru kenyatta kupitia arifa maalum ya gazeti rasmi la serikali Edwin Abonyo atakuwa mwanachama wa kamati hiyo kwa miaka mitatu ijayo. Abonyo ni miongoni mwa watu saba walioteuliwa .kwingineko waziri wa leba Ukur Yattani amemteua mbunge wa zamani wa Othaya Mary Wambui kuwa mwenye kiti maamlaka ya kitaifa ya ajira kwa kipindi cha miaka mitatu .
Wenye magari watapata afueni mwezi huu baada ya mafuta ya petroli na diesel kupungua kwa mujibu wa tathmini mpya iliyotangazwa na tume ya Petroli na kawi . lita moja ya petrol hapa jijini itauzwa kwa shilingi 108 Nukta 05 kutoka shilingi 112 na senti 81 .lita moja ya disel itauzwa kwa shilingi 101 na senti 96 kutoka bei ya awali ya shilingi 103 nukta 03 . bei ya mafuta taa hata hivyo imepanda hadi shiingi 101 nukta 08 kutoka shilingi 100 na senti 64 .
Bunge la Kaunti ya Busia ndilo la hivi punde kuukata mswada wa punguza mizigo uliopendekezwa na chama cha Thirdway Alliance .waakilishi wa kaunti wamesema wananchi hawakuhusishwa katika kutayarisha mswada huo na vile vile utarejesha nyuma hatua zilizoafikiwa kufanikisha ugatuzi .
Chuo kikuu cha Moi Kimewafurusha viongozi watano wa wanafunzi ambao wanadaiwa kupanga maandamano yaliokumbwa na ghasia wiki jana na kusababisha chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana . naibu chansella Isaac Kosgey amethibitisha kwamba wanafunzi hawatakubaliwa kurejea shuleni humo .
Mahakama moja mjini Voi imempata na hatia mwanamume mwenye umri wa miaka 56 aliyembaka bintiye mwenye umri wa miaka 17.Mwemba Gereza anadaiwa kutekeleza kitendo hicho Agosti 28 mwaka 2016 katika eneo la Buguta huko Voi.Hakimu mkaazi wa Voi Fredric Nyakundi amesema upande wa mashtaka ulidhibitisha kuwa mshukiwa alitekeleza kitendo hicho cha kinyama
Familia za wakenya waliofariki katika ajali ya ndege ya Ethiopia hatimaye zimekubaliwa kuichukua miili ya wapendwa wao . waziri wa mashauri ya kigeni Monica Juma amesema miili yote imetambuliwa huku 28 ikiwasili nchini kwa maazishi ilhali iliosalia itachomwa.miili mingine ya waliokuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja itazikwa kwa mujibu wa matakwa ya familia .
Wazazi wameshauriwa kukoma kuwapa shinikizo wanafunzi kufanya vyema katika mitihani ya kitaifa .waziri wa elimu George Magoha pia amewataka watahiniwa wa mwaka huu kutoitikia kuwekwa chini ya shinikizo kwani kila mmoja atasonga katika hatua ifuatayo ya elimu bila kujali matokeo yake .
TSC imewapiga marufukua walimu waliohusika na visa vya udanganyifu katika mitihani ya hapo awali dhidi ya kusimamia mitihani ijayo ya KCPE na KCSE . Afisa mkuu wa tume hiyo Nancy Macharia amesema katika miaka mitatu iliyopita ,wamewachukulia hatua walimu 144 waliohusika na udanganyifu katika mitihani ya kitaifa .
Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kaunti ya Nairobi Abdi Guyo ameandikisha taarifa na DCI akidai kamba maisha yake yamo hatarini . Amesema kizazaa kilichotokea city hall wiki jana kilipangwa na magenge yalitumwa katika bunge la kaunti kusambaratisha shughuli .
Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za marathon Eliud Kipchoge ametaka kukutana na rais wa zamani wa marekani Barrack Obama .hii ni baada ya Obama kumtumia ujumbe wa kumhongera katika twitter kwa kumudu kumaliza mbio za marathon chini ya saa mbili .Obama pia alimtambua Brigid Kosgei kwa kuvunja rekodi ya akina dada katika mbio za marathon..Kipchoge anataka kukutana na Obama ili kujadili jinsi ya kuufanya ulimwengu kuwa bora zaidi .
SERIKALI imeshtakiwa kwa kuondoa paspoti za kidiplomasia za majaji wa mahakama kuu na kuwazuia kutumia maeneo ya watu mashuhuri katika viwanja vya ndege . mkenya ,jonathan Munene amesema hatua hiyo inatishia uhuru wa idara ya mahakama na nataka arifa hiyo ya kisheria kufutiliwa mbali .
Waziri wa usalama wa ndani Fred matiangi amefutilia mbali likizo ya maafisa wakuu wa polisi ili waweze kuangazia kikamilifu mitihani ijayo ya kitaifa . matiangi pia amewahakikishia wakenya kwamba hapatakuwa na udhaifu wa kiusalama wakatai wa mitihani hiyo.
Watoto wa Kenya ni werevu na hawahitaji kushiriki udanganyofu ili kupita mtihani .waziri wa elimu George magoha amewatahadharisha walimu ,wazazi na maafisa wa elimu ambao huenda wana njama ya kujaribu kuwasadia wanafunzi kufanya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa .
Usijaribu kuyatumia maneno ya kujifanya ni kama unafahamu wanayopitia watu wenye maradhi kama vile kansa au kuwamabia kwamba kila jambo hutendeka kwa ajili ya sababu Fulani . mwanasaikolojia Riziki Ahmed amesema matamshi kama hayo huwavunja moyo wagonjwa hao.
Video ya dakika 47 iliyorekodiwa ya Peter Ngugi aliyekuwa akiwapasha polisi habari akikiri kuhusika na mauaji ya wakili Willie Kimani haitachezwa kortini .jaji amesema afisa aliyerekodi video hiyo hakufutwa kanuni zifaazo wakati wa kuichukua video hiyo iliyofaa kutumiwa kama ushahidi .
Miili ya wakenya walioaga dunia katika ajali ya ndege ya shirika la Ethiopia airlines imewasili katika uwanja wa ndege wa JKIA ili kuchukuliwa na jamaa zao .miili 28 kati ya 32 ya wakenya hao walioafriki katika mkasa huo imewasili mapema leo katika uwanja huo .watu 157 waliangamia katika ajali hiyo mwezi machi .
Uhaba wa walimu huko taita taveta unachangia kudorora kwa ubora wa elimu .mbunge wa mwatate Andrew Mwadime aniataka tume ya kuwajiri walimu TSC kuwaajiri walimu zaidi katika eneo hilo kwani kuna vijana wengi waliohitimu kuwa walimu lakini hawana kazi .
Mbunge wa kitui mashariki Nimrod Mbai anataka kamishna wa kaunti ya Kitui John Ondego ahamishwe kwa madai ya kukosa kurejesha hali ya usalama katika eneo hilo linaloshambuliwa mara kwa mara na wafugaji wa ngamia . Mbai amesema wenyeji sasa wamelazimika kuishi katika kambi za muda ilhali serikali haijachukua hatua zozote madhubuti za kuwalinda .Odengo hata hivyo amekana kuwyatelekeza maslahi ya wakaazi hao.
Chama cha ODM kimetakiwa kuwahakikishia wakenya kwamba kitadumisha amani wakati wa uchaguzi mdogo wa kibra .mbunge wa kiharu Ndindi Nyoro amesema kisa kama kilichotokea mwishoni mwa wiki ambapo msafara wa mgombeaji wa Jubilee Mcdonald mariga ulishambuliwa kwa mawe sio jambo linalofaa kukubaliwa .
Serikali itazidisha mara dufu jitihada za kukabiliana na udanganyifu katika mitihani ya kitaifa mwaka huu .afisa mkuu mtendaji wa baraza la kitaifa la mihani Mercy Karogo amewashauri maafisa wakuu wa elimu katika kaunti ndogo kuhakikisha kwamba wanafuatilia kikamilifu usimamizi wa zoezi la mtihani katika maeneo yao .
Wakaazi wa Mombasa wanaitaka serikali kuboresha usalama katika feri ili kuzuia maafa siku za usoni . wamesema baadhi ya sehemu za feri zinafaa kuboreshwa na pia kuweka vifaa vya kuwawezesha watu kujiokoa wakati panapotokea dharura .