Mlinzi wa usiku auawa Kwale

Polisi wanalisaka  genge la majambazi  waliomwua mlinzi mmoja huko Ukunda, Kwale kwa kumkatakata na kisha kuiba kompyuta mbili katika afisi aliokuwa akilinda.

Kamishna wa kaunti ya Kwale Kutswa Olaka  amesema wanachunguza mauaji hayo  na iwapo yanayahusiana na  vita dhidi ya washukiwa wa  biashara ya dawa za kulevya.