Mohammed Ali awasilisha mswada wa kumtimua waziri wa Uchukuzi

Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amewasilisha mswada wa kutaka atimuliwe waziri wa Uchukuzi na miundomsingi Jmaes Macharia kwa madai ya kukiuka katiba.

“Cabinet Secretary James Macharia has failed to set up crucial infrastructure such as highways, bridges, ports and airports despite such projects being hailed as important for the country’s economic growth,” unasoma mswada huo.

Ali anamkashifu pia Macharia kwa madai ya ufisadi kutokana na mradi wa ujenzi wa nyumba katika kaunti ya Nairobi ambao ulistahili kusimamiwa na kampuni ya Suraya Property Limited ambayo kulingana na Ali inamilikiwa na Macharia.

Amesema kuwa waziri huyo anapania kulemaza shughuli za ukuaji wa majimbo ya Pwani nchini baada ya kuagiza mizigo yote kusafirishwa na reli ya kisasa SGR , jambo ambalo litawanyima wakaazi wa maeneo hayo posho.

“This has caused a lot of public suffering in the transport sector which has led to many businesses closing down and loss of over 100,000 jobs,” reads the petition. “It is very annoying that the Cabinet Secretary continues to ignore stakeholders in the implementation  ministry projects.”

 Ali amekashifu agizo hilo akisema ni kinyume na haki za wakenya ambao wanastahili kunufaika na bandari ya Mombasa.