Monicah Kimani: Jowie Irungu aachiliwa kwa dhamana ya milioni 2

Joseph Irungu almaarufu Jowie ameachiliwa huru kwa dhamana ya kitita cha shilingi milioni 2 katika kesi ya mauji ya mwanabiashara Monicah Kimani.

Jowie aliachiliwa huru siku ya alhamisi na mahakama ya Milimani.

Jaji James Wakiaga alisema hakuna sababu ya kumnyima mshtakiwa dhamana akiongeza kuwa tayari hali zimebadilika.

Mashahidi ambao walikuwa chini ya ulinzi tayari wametoa ushahidi wao.