Zari hassan amuomboleza mkewe meneja wa Diamond Babu Tale

_4ek9kpTURBXy9kMTZlNWE4YzczYzJiNTBiMDRkMDNhOWI0NmU0MmM2ZC5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB
_4ek9kpTURBXy9kMTZlNWE4YzczYzJiNTBiMDRkMDNhOWI0NmU0MmM2ZC5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Zari Hassan amemuomboleza mkewe meneja wa staa wa bongo Diamond Babu Tale baada ya kuaga dunia Jumapili huku habari za kifo chake zikiwashangaza wengi.

Zari alikuwa rafiki wa karibu wa Shamsa Kombo Tale, kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Instaram Zari alimsifu mwendazake Shamsa kwa kuwa mtu mwenye roho nzuri.

"Pole sana Babu @BabuTalee, we mourn with You. It is hard to believe yet it’s a fact. And just like that you are gone. My heart bleeds for your kids Shammy. But one thing I know, God still reigns. He will take care of them, only Him can do the best. Rest in Peace sister

Mothers die with the most pain; Lil girl isn’t even 3 years. Her mama is no more. Help me come together and pray for @BabuTale family. As a mother I’m so devastated #RIPShammy

I will miss you so much, your soul was pure. God wanted an angel for himself. Rest Easy Babe." Aliandika Zari.

Kulingana na ndugu yake Babu Shamsa alikuwa anaugua malaria na vindonda vya tumbo na hali yake ya afya ilidhoofika mnamo Jumamosi na kupelekwa hospitalini.

Baada ya kufikishwa hospitalini alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, marafiki, jamaa na hata wasanii mbalimbali walituma risala za rambirambi zao na hizi baadhi ya jumbe zao;

 Aunty Ezekiel:Yaani Sijui lakini Nawaza Watoto Jaman Familia yako imevunjika gafla jaman ni Hali gani watoto watakuwa nayo Mungu wangu......😭😭😭Kwake ni Mwanzo na Mwisho wote tutarejea Pumzika kwa Amani Shammy wangu Dada Mwenye Upendo Dah!😭😭😭.Pole Sana Boss Talle.....Inshallah Mwenyezi Mungu akufanyie Wepesi kwenye Muendelezo wa Familia yako 😔😥😥😥

Nandy:Poleni sana ndugu jamaa na marafiki kwa msiba uliotokea BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE! MUNGU akutie nguvu boss 🙏🏻

Chege Chigunda:Inna lillah wainna ilayhi raaj un!pole sana sana Boss tale wewe pamoja na familia yako kwa kuondokewa na Mkeo,Allah akutie nguvu bro njia yetu sote ni moja kaka Allah amuweke mahala pema🙏”

MHARIRI; DAVIS OJIAMBO