Mpira Ukipita Dakika 90 Basi Ni Bahati Nasibu, Alalamika Gidi Shabiki Wa Ufaransa

ufaransa
ufaransa
Siku ya Jumapili, Ureno ilistaimili kumpoteza nahodha wao Cristiano Ronaldo mapema katika mchuano wa fainali ya kombe la euro ili kushinda taji hilo kwa bao moja la dakika za muda wa ziada kwa hisani ya mchezaji Eder, taji la kwanza la kimataifa la taifa hilo.

Baada ya taifa hilo kuandikisha historia dhidi ya wenyeji ambao walikuwa wamepigiwa upato mkuu kutwaa taji hilo, mtangazaji Gidi Gidi alikuwa mwingoni mwa mashabiki waliohuzunika zaidi.

Gidi shabiki sugu wa ufaransa alikerwa na matokeo haya siku chache tu baada ya kujivunia ushindi wao dhidi ya Ujerumani katika nusu finali za michuano hayo akidai kuwa hatopoteza gari lake la Mercedes Benz, laiti angalijua kuwa kichapo chamngoja.

"Ni Monday freshi kabisa, ingawa sio freshi kwa watu wengine kama mimi kwa sababu timu yangu ya Ufaransa ilipoteza fursa ya kunyakua kombe la Uropa". Alisema Gidi huku akifungua kipindi cha Gidi na GHost asubuhi.

"Lakini mimi huwa nasema ya kwamba, mpira ukipita dakika 90 hiyo nyingine ni bahati nasibu." Aliongeza Gidi huku akiwapongeza wareno kwa ushindi wao mkuu licha ya kuwa na uchungu mwingi.

Skiza kanda ifuatayo.