Msaidizi afutwa kazi kwa kutoa taarifa za siri za familia ya Trump

trump
trump

Msaidizi binafsi wa rais wa Marekani Donald Trump'amelazimishwa kujiuzulu kutoka White House baada ya kujulikana kimakosa kwa taarifa nzinazoihusu familia ya Trump

Madeleine Westerhout, mwenye umri wa miaka 29, aliondolewa kazini ghafla w siku ya Alhamisi baada ya rais kubaini kuwa amekuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa chakula cha jioni mwezi huu .

Alikuwa akinywa pombe na kujisifu kuhusu namna anavyoweza kumfikia rais Trump wakati wa mapumziko ya New Jersey, kimeripoti kituo cha habari cha CBS News

Bi Westerhout alifanya kazi na Trump tangu siku yake ya kwanza ya urais.

Ikulu ya White House imekataa kutoa kauli yoyote juu ya kufutwa kazi kwake.

Gazeti la New York Times, ambalo liliripoti kwa mara ya kwanza juu ya kufutwa kazi kwa Westerhout , lilisema kuwa chanzo cha habari cha White House alisema kwa sasa anachukuliwa kama "mfanyakazi aliyetengwa " na kwamba atazuiwa kurejea katika ikulu hiyo Ijumaa.

Akielezewa na vyombo vya habari vya Marekani kama mlinzi wa lango la Trump , Bi Westerhout alikuwa na ofisi yake mkabala na ofisi ya rais inayofahamika kama Oval Office katika jengo la West Wing.

Kauli zake anazoshutumiwa kuzitoa kwa wandishi wa habari alizitoa wakati wa chakula cha jioni na hazikuwa zinarekodiwa wakati alipokuwa akizungumza na maripotoa katika hoteli ya Berkeley Heights, New Jersey, wakati Bwana trump alipokuwa mapunzikoni katika klabu yake iliyopo Bedminster, New Jersey, mapema mwezi Agosti.

Vyanzo vya habari vimeiambia CBS News kuwa alikuwa akinywa pombe na akatoa taarifa kuihusu familia ya rais. Pia ameripotiwa kutoa taarifa za uvumi kuwahusu watangazaji wanaotaka kumuona rais.

haijafahamika ni vipi Trump alifahamu mazungumzo hayo yote.

-BBC