gun

Mshukiwa wa kuuza bangi apigwa risasi Bungoma

Maafisa wa polisi na wale wa upelelezi huko Bungoma wamempiga risasi na kumuua mshukiwa mmoja wa kuuza bangi katika mtaa wa Moca eneo la Mandizini mjini Bungoma

Isaack Ngongu ambaye anamiaka 36 na ni baba ya watoto watatu alipigwa risasi tatu moja kuifuani na mbili shingoni na maafisa hao amabo walikuwa wakifanya msako dhidi ya washukiwa wa kuuza mihadarati inje ya nyumba yake hapo jana usiku.

Mama alimuuza mtoto wangu kwa shillingi 35,000

Mkuu wa upeplezi kauntyi ya Bungoma amesema kwamba maafisa wake wameanzisha msako dhidi ya watu ambao wanauza madawa ya kulvta eneo hilo.

Aidha familia ya mwendazake imekashifu maauji hayo na kuomba maafisa wa IPOA Kuingilia kati na kuwapa haki kwani mwanao hakua jambazi bali alliukua tu anauza bangi.

Kwingineko, biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Ojame Adungos kaunti ndogo ya Teso Kusini kaunti ya Busia baada ya mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu kuangukiwa na mti na kufariki papo hapo.

Utabiri wa mechi katika ligi kuu ya Uingereza

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatau katika chuo kikuu cha Nairobi Maurice Okware, mwenye umri wa miaka 23 alikuwa anakata mti huo kuchoma matofali ili apate karo ya shule wakati ulimuangukia na kumuua papo hapo alipojaribu kuuzuia usiangukie nyumba ya jirani.
Wazazi wake Charles Ariku na Magdalene Akwenyat na majirani wametaja kifo cha mwanafunzi huyo kama pigo kubwa kwa familia hiyo wakimtaja kama mwenye bidii na mwerevu.

Ruto kama Donald Trump. Jinsi anavyotumia Twitter kukashifu habari ‘feki’

-Brian Ojamaa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments