Mshukiwa Wa Utekaji Nyara Na Ubakaji Akamatwa Migori

Polisi wamemkamata mwanamume  anayedaiwa kuwabaka na kutekanyara wanawake na wasichana wadogo mjini Awendo.

Kwa mujibu wa afisa wa upelelezi wa kaunti ya Migori Benedict Kigen, mshukiwa huyo Calvince Owino Hilda alikamatwa na polisi wakishirikiana na umma akituhumiwa kuwatekanyara na kuwabaka wanawake katika mashamba ya miwa maeneo ya Awendo na Uriri.

Mshukiwa  atafikishwa mahakamani baadaye kujibu mashtaka huku polisi wakiendelea kuwatafuta wenzake wanaoaminika kushirikiana naye katika uhalifu huo.