Mshukiwa Wa Wizi Achomwa Bondo

Wingu la simanzi limetanda katika kijiji cha Aber eneo la Bondo baada ya wachukuzi wa boda boda kumuua mwanaume mmoja kwa jina Michael Juma.

Kulingana na baadhi ya wanafamilia, wachukuzi hao wa walivamia nyumba ya Juma majira ya saa tano usiku na kumdunga kisu tumboni kabla ya kumchoma.

Inadaiwa kuwa wachukuzi hao wa  waligadhabishwa na Juma baada ya kutajwa miongini mwa wale waliotekeleza mauji ya jirani yake baada ya kutoweka na mke wa mjombake.

Akithibitisha kisa hicho chifu wa eneo hilo Patrick Obilo alielezea kuwa marehemu alidungwa na kisu tumboni mara kadhaa kabla ya kuchomwa na mwili wake kutupwa katika mlango wa mamake ukichomeka.

-Lameck Baro