Mshukiwa Wa Wizi Wa Ng'ombe Auwawa Bungoma

death
death
Wakaazi wa kijiji cha Kitinda eneo la Sang'alo katika eneo bunge la Kanduyi kaunti ya Bungoma wamemuua kwa kumpiga mshukiwa mmoja wa wizi baada ya kupatikana na ng'ombe wa wizi usiku wa manane.

Inasemekana kuwa mshukiwa mwenye umri wa makamu alikuwa amemuiba ng'ombe huyo eneo hilo na alikuwa anaelekea naye sehemu ya Bukembe ambako yeye pia anatoka.

Akithibitisha kisa hicho naibu wa chifu wa sehemu hiyo Robinson Barasa amesema kuwa tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.

-Brian Ojamaa