Mtangazaji Gidi Aunganisha Wakenya Na Watalii Kupitia Wimbo Wa Kogalo Nchini Ufaransa (VIDEO)

Mtangazaji wa Radio Jambo, Gidi Gidi anajulikana sana kwa umahiri wake katika nyanja ya uanahabari kwani kipindi chake cha Gidi na Ghost Asubuhi ndicho kipindi nambari moja nchini, katika mida ya asubuhi.

Gidi ambaye pamoja na mwenzake Ghost Mulee huwa na kitengo cha Patanisho ambacho huleta pamoja wawili waliokosana na kuwapatanisha, haswa wanandoa.

Basi mbali na shughuli za utangazaji, Gidi ni mpenzi wa kandanda huku akijulikana kwa kuwa shabiki sugu wa timu za Gor Mahia na Arsenali ambazo zachezea ligi za Uingereza na Kenya mtawalia.

Gidi hajakuwa katika studio katika mda wa majuma mawili kwani alisafiri ng'ambo pamoja na mwenzake Mulee katika shughuli za kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe, Marie-Rose Hera Ogidi, ambaye alikuwa anasherehekea mwaka mmoja.

Baada ya sherehe Gidi aliandamana na mwenzake pamoja na familia yake kushabikia timu ya raga ya wachezaji saba kila upande ya Kenya, katika mashindano ya raga mjini Paris.

Kama ilivyo desturi, mashabiki wa Kenya ndio wanaojulikana kwa shamra shamra na mbwembwe chungu nzima katika michuano hii na basi ilikuwa fursa bora kwa watangazaji hawa pindi tu walipoungana na wakenya wenzao.

"Kogalo, Goooor....Gor Mahia..

"Kogalo, Goooor..Gor Mahia...

"Pinje duto ywakni, Gor..Mahia...

Katika hali ile ya kushangilia wachezaji wa Kenya, Gidi alitumia fursa ile kuimba wimbo mashuhuri wa kuisifu timu ya Gor Mahia.

Katika harakati ile, Gidi na Ghost waliwafurahisha watalii ambao pia waliungana nao na kuisifia Gor Mahia.

Tazama kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be