Mtangazaji wa siku za kale? Marie-rose atembelea studio zetu!

Mwanawe mpendwa wa mtangazaji, Gidi Ogidi, Marie-Rose Hera Ogidi alizitembelea studio zetu siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza, huku akiandamana na mamake.

Mbali na kupiga picha na mtangazaji Ghost Mulee na babake ndani ya studio, Marie-Rose alipata fursa murwa ya kuketi katika kiti ambacho babake huketi na kuskizwa na mamilioni ya wakenya duniani kote.

Huku akiwa amevishwa headphones, Marie-Rose alijihisi kama mtangazaji gwiji na alipata fursa ya kuzungumza (ingawa hakuwa hewani) huku akiwasalimu na kujitambulisha kwa 'wananchi'.

Gidi alichapisha video na picha za mwanawe akiwa studioni huku akiwatumbuiza kwa dakika kadhaa kabla ya kuondoka.

Je siku moja Marie-Rose ataja kuwa mtangazaji waku enziwa na mamilioni mwa wakenya kama babake? Hayo ndio matumaini yetu kwa sasa.

Katika pilka pilka hizo, rafikiye Gidi, Maina Kageni ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Classic 105, alimuandalia keki tamu ya kumkaribisha tena nchini Kenya.

Marie-Rose amekuwa nchini kwa wiki kadhaa sasa baada ya shule kufungwa kwa msimu wa majira ya joto. Miongoni mwa vitu amekuwa akifanya humu nchini ni kutembea maeneo kadhaa na babake.

Hivi majuzi wawili hao walijipata katika mabishano ya kukata na shoka, baada ya mwanawe Gidi, kukiri kwamba unapaswa kutamka mfuko kama 'Popet' kwa kimombo badala ya 'pockets'.

Tazama picha na video zifuatazo.

https://www.instagram.com/p/B1G8Z_oAHEX/