Murder

Mtoto auwawa na babake mdogo kwa jembe

Wananchi katika kijiji cha madende kaunti ndogo ya nambale kaunti ya busia wameachwa vinywa wazi baada ya mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 27 kukata kichwa cha mtoto mvulana mwenye umri wa miaka minne wa nduguye na kuanza kutembea nacho barabarani.

Kulingana na ocpd wa nambale Robert Ndambiri na chife wa kata hiyo Gerishom Wandera Pate, mwanamme huyo mwenye akili taahira alimtaka mtoto huyo kichwa kwa kutumia jembe kabla ya kwenda nacho barabarani.

Hata hivyo wananchi walimrejesha kwa boma alikotendea kitendo hicho cha unyama na kumjeruhi kichwani kutumia jembe lilo hilo.

Maafisa wa polisi waliondoa mwili wa mtoto huyo pamojana jamaa huyo akiwa hali mahututi lakini akaaga dunia alikokuwa anapelekwa hospitalini.

Leornard Acharry Ojiambo

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments