Mtu mmoja afariki kutokana na ajali mbaya katika barabara ya Lang’ata

unnamed (1)
unnamed (1)

Mtu mmoja alifariki katika ajali kwenye barabara ya Lang’ata jijini Nairobi.

Polisi wanasema huenda mwendazake alikuwa mlevi alipokuwa akiliendesha gari lake kutoka hoteli ya Weston.

Gari lake lilibingirika mara kadhaa Kabla ya kuwaka moto kabla ya kuingia kwenye ua wa uwanja wa ndege wa Wilson karibu na shule ya upili ya Sunshine.

Hayo yakijiri, msaidie mwanao kufahamu kuwa kanuni unazompa anapotumia mtandao na wakati hautumii zinastahili kudumishwa saa zote.

Mtaalamu wa masuala ya kimitandao Bright Gameli anakushauri kumfunza kufikiria kwa umakini kabla ya kuweka maarifa yao au kuanza urafiki na mtu yeyote  kwenye mitandao ya kijamii.

Kwingineko, je ni mambo yepi ambayo rafiki zako wanafahamu kuhusu uhusiano kati yako na mpenzi wako?

Mtaalamu wa uhusiano Cylus Kiriinya  anakushauri kutokuwa na mazoea ya kuweka mambo yenu ya ndani zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwani huenda yakawapelekea kuchokozwa chokozwa.