Mtu mmoja afariki watatu wajeruhiwa baada ya gari kubingitia Lamu

Mtu mmoja alifarki papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya gari walimokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kubingiria mara kadhaa eneo la Hindi, Lamu magharibi Jumapili jioni.

Majeruhi wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya King Fahad mjini Lamu.

Mwenda zake Yusuf Abdisaman 31, anasemekana kuliendesha gari hilo kwa kasi mno kabla ya ajali hiyo kutokea.

Walioshuhudia walisema dereva huyo alionekana kung’ang’ana na usukani kabla ya kulazimika kutumia breki za dharura hali iliyosababisha gari hilo kupoteza mwelekeo na kubingiria.

Kamishna wa kaunti ya Lamu Joseph Kanyiri amedhibitisha ajali hiyo na kuwataka wenye magari kuwa makini wanapotumia barabara eneo hilo hasa msimu huu wa mvua na utelezi mwingi ili kuepuka maafa.

-CHETI PRAXIDES