Mtu Mmoja Apigwa Risasi Na Maafisa Wa Polisi Na Kufariki Huko Bungoma

bungoma
bungoma
Mtu mmoja mwenye umri wa makamu ameuawa mapema leo mjini Bungoma katika eneo la Muteremuko eneo bunge la Kanduyi kwa kupigwa riasi na maafisa wa polisi.

Jamaa huyo ambaye ni fundi wa viatu katika barabara ya Bungoma kuelekea mjni Mumias alikua miongoni mwa watu waliuokuwa wakitoroka baada ya rabsha na vita kuzuka baina ya vijana na maafisa wa polisi.

Vijana hao walikua wamewasha moto na kuzua rabsha kutokana na uchaguzi wa hapo jana

Kamishna wa kaunti ya Bungoma, Joshua Chepchieng amesema kwamba maafisa wa polisi wanawazuilia watu tano waliozua rabsha mjini humo jana usiku.

Amewaonya wakaazi dhidi ya kuzua rabsha na kudai kwamba yeyote atayepatikana atachukuliwa hatua kali za kisheria.

-Brian Ojamaa