Mudavadi awarai viongozi kuacha siasa za mgawanyiko

Mudavadi
Mudavadi
Kiongozi wa ANC  Musalia Mudavadi  amewataka viongozi wa kisiasa kukoma  kuendeleza siasa za mgawanyiko  ambazo huenda zikalihatarisha  taifa  tunapoelekea uchaguzi wa mwaka wa 2022

Mudavadi  amesema wakenya wanafaa kukumbuka kwamba maelfu ya wakenya walipoteza maisha yao  kwa sababu ya siasa kama hizo . Amesema alikuwa miongoni mwa viongozi waliohusika na mazungumzo ya kuleta Amani nchini wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007.

Mudavadi  amesema  ni ukosefu wa uajibikaji  kwa viongozi  kutumia matusi  ili kuzua mgagawanyiko  wa kikabila .

" Tuheshimu  maoni ya kila mmoja . hakuna aliye na haki ya kumtukana mwenzake . Mbona mtu amlenge  mama  Ngina  kisiasa?’ Musalia alihoji  kuhusu matamshi aliotoa mbunge wa  Oscar Sudi na mwenzake  Johana Ng’eno .

Mudavadi amesema  Umoja wa  sio jambo linalofaa kuibngizwa mzaha  kwani ustawi wa taifa unategemea umoja wake .

Mudavadi  aliyazungumza hayo katika shule ya msingi ya  Gaitheri huko kiharu  wakati wa mazishi ya  mwakilishi wa wadi ya Gaturi Kiiru Mwangi kwa jina maarufu  Mbembe aliyeaga dunia wiki jana .