Muhubiri tata James Ng'ang'a ahusishwa na skendo ya ardhi

v8FEzbqdLrnganga__1576405445_24852
v8FEzbqdLrnganga__1576405445_24852
Muhubiri mwenye utata James Ng’ang’a anatuhumiwa kujenga kanisa katika sehemu ya ardhi inayomilikiwa na Susan Ngina Kanyali.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Nation, Susan anahoji kuwa ameiandikia bodi inayoshughulika na maswala ya ardhi kaunti hiyo ila aweze kupata haki zake.

 Mwanadada huyu anasema kuwa tume ya ardhi nchini ilimpa hatimiliki za sehemu hiyo ya ardhi.

Bodi ya kaunti inadaiwa kumwandikia Ng'ang'a barua ya kukoma shughuli za ujenzi katika kipande hicho cha ardhi.

Aidha Susan amesema kuwa chifu wa eneo lao Mohammed Dida amemtishia na kusema kuwa hana uwezo wowote wa kifedha unaomuwezesha kufuata kesi hiyo.

Dida hajaweza kutoa kauli kuhusu usemi huo kwani kesi hiyo imewasilishwa mahakamani.