Mungu wa Ajabu! Size 8 na Dj Mo wakaribisha mtoto wa pili

DJ Mo na Size 8 wamebarikiwa na hivi juzi walikaribisha mtoto wao wa pili na mama pamoja na mtoto wako salama salmini.

Juzi Size 8 aliweka video ya kibonzo kwenye mtandao wa kijamii na kuandika ujumbe wa kumshukuru Mungu kwa baraka tele. Aisee Mungu hamuachi mja wake

"My victory dance. Some good news, thank you, Jesus. Waa, Jesus, you are faithful," Size 8 aliandika.

Zaidi ya hayo, Dj Mo aliweka video kwenye mtandao wa kijamii ya mtoto wao Ladasha na Size 8 akiandika,

"Thank you DJ Mo for this, when I can't really be there for her."

Dj Mo naye akasema,"Viatu zake amesema zikae hivo na tusimletee watoto."

Hata hivyo, Dj Mo anatakiwa kuwahakikishia mashabiki kuwa walipata mtoto na pia watujuze walipata mtoto wa jinsia ipi.

Ni furaha sana kwa familia hii kwani wapenzi hawa walifunguka na kueleza walivyo sikitika baada ya kupoteza mtoto wao wa pili.

"My wife was five weeks pregnant before the miscarriage. Miscarriage can be caused by so many things, like stress. Others may fail to adjust with the body, but we are doing well," Alisema.

Kama Radio Jambo tunawapongeza wapenzi Dj Mo na mke wake mpendwa Size 8 kwa kuleta zawadi nono kutoka mbinguni na tunamtakia mema yote waendeleapo kuwalea watoto wao.