Murkomen aapa kupinga mswada wa ugavi wa mapato ya taifa

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen ameshikilia msimamo wake kwamba atapinga mfumo unaopendekezwa wa ugavi wa mapato ya kitaifa.

Katika taarifa yake siku ya Jumatatu Murkomen alisema kwamba msimamo wake dhidi ya mfumo unaoungwa mkono na uongozi wa wengi katika seneti umevutia maswali mengi na ilhali kaunti yake ni moja wapo wa kaunti ambazo zitanufaika ikiwa mfumo huo utatumika.

Soma habari zaidi;

"Nataka kueleza msimamo wangu na ule wa maseneta wenzangu  Cleophas Malala (Kakamega), Mithika Linturi (Meru), Johnson Sakaja (Nairobi), Boniface Kabaka (Machakos) na wengine wengi unatokana na uamuzi wetu binafsi kuwa mgao wa mapato ya taifa haufai kuwa mchezo ambapo kaunti zingine lazima zipate na zingine zipoteze ,” Murkomen alisema.

Seneta huyo ambaye alibadumduliwa kutoka wadhifa wa kiongozi wa wengi alisema kwamba wenzake kama vile kiranja wa wengi Irungu Kang'ata wanaohoji msimamo wake wanaashiria sura halisi ya ubinafsi na kujipendelea kwa wanasiasa nchini.

Soma habari zaidi;

Huku wakenya wakisubiri kuona vile seneti itatatua utata unaozingira hoja hiyo leo Jumanne Murkomen amesema kamwe hataunga mkono mfumo ambao utawanyima haki baadhi ya wananchi.

“Sitaweza kwa dhamira yangu, kuunga mkono mfumo ambao unalenga kupokonya kaunti ndogo zenye raslimali chache na ambazao zilikuwa zimetengwa...ili tu kaunti yangu ya Elgeyo Marakwet ifaidike leo, ni hizi kaunti zilizotengwa ambazo zimewekwa kwenye kichijio, lakini kesho itakuwa Elgeyo Marakwet," aliongeza.

Soma habari zaidi;

Alisema maseneta wanafaa kuangazia swala la kushinikiza serikali kuu kuongeza mgao wa serikali za kaunti badala ya kuunga mkono hoja inayozinyima baadhi ya kaunti pesa.

“Hilo ndilo jukumu letu na sio kufilisisha baadhi kaunti zetu. Hatua hii ni sawa na kaka kumuibia Peter na kumlipa Paul.”

Murkomen aliongeza kuwa swala hilo linaweka umoja wa kitaifa kwenye mizani.

Wakenya wanasubiri kwa hamu kuona kama seneti itatatua utata huo ama hoja hiyo tena itaahirishwa kwa mara nane.