Musa aeleza alivyopigiwa simu kuokoa maisha mkasa wa feri Likoni, adai mkataba

thumb_kdcbwledgdih5ac861fb0fbc2
thumb_kdcbwledgdih5ac861fb0fbc2
Baada ya tukio la gari kutumbukia Bahari Hindi Jumapili, mpiga mbizi kwa jina Musa amefunguka A-Z alivyopigiwa simu kuokoa maisha.

Nchi nzima iligutushwa na taarifa kuwa Mama Mariam Kighenda, 35, na mtoto  wake Amanda Mutheu, 4 wamezama na kufa maji Likoni.

Wawili hawa walikuwa wanatoka kukagua shamba lao Kwale katika gari lao la Toyota KCB 289C .

Musa anasimulia masaibu anayokumbana nayo anapotaka kuajiriwa katika huduma ya feri kuokoa maisha.

Soma hadithi nyingine;

"Hiki kisa cha leo nipo nyumbani napigiwa simu. Napigiwa simu watu wametumbukia ndani ya maji washakufa already..."

'Nami mpaka dakika hii hizi kazi nimezifanya nyingi sana na sioni matunda yake. Nishafanya hii kazi ya diving mpaka nikasalimia malkia kwa mkono wangu..."

Musa ambaye amebobea katika upigaji mbizi anasema kuwa hapewi heshima inayostahili,

"Nikirudi hapa sherehe zinafanyika kubwakubwa. Juzi Uhuru alikuja kufungua Blue Economic hapa,nilizuiliwa mpaka kuingia huko ndani."

"Saa hizi mtu anakufa maji huku naaanza kupigiwa simu Musa yuko wapi."

"Na wengi nimewatoa ndani ya maji hawana hesabu mpaka sasa hivi nimechoka na thawabu..."

Soma hadithi nyingine;

"Nikona vijana na wengi sio time yote Musa. Musa akifa mwingine atatoka wapi? Vijana wapatiwe kazi wafanye hii kazi."

"Tukijaribu njia zote tuajiriwe tunaambiwa tusubiri. Saa hii sitaki niingie ndani ya maji kama musa wa zamani,naingia na mkataba."

Musa anateta kuwa anahitaji mkataba na bima ya maisha yake ili kuweza kuanza kufanya juhudi za kukokoa maisha katika bahari.

Lucy Rajula ambaye ni dada wa mume wa Kighenda alisema kuwa ilikuwa desturi ya John Wambua (mumewe Mariam) kumpa gari mkewe azuru shamba Likoni.

“Alikuwa amesalia nyumbani na kijana wake huku bibi ameenda na gari.” Lucy Rajula.

Soma hadithi nyingine;

Kulingana na Lucy, Kighenda alikuwa anaendesha biashara ya kuuza nguo.

Picha kwenye mitandao zinaonyesha kuwa Mariam alikuwa mchangamfu.

Alipenda fasheni na alikuwa mwenye furaha tele.

Familia ya John Wambua na Mariam iliishi maisha ya furaha kwa mujibu wa picha hizo.

Walimu wa shule ya msingi ya MM Shah walisema kuwa Mutheu alikuwa mwanafunzi mchangamfu.

‘Alikuwa mwenye furaha siku zote. Alikuwa mwerevu zaidi. Inauma kumzungumzia…,” Alisema mwalimu wake.