Kati ya mwaka wa 2002 na 2007 Kagwe alihudumu kama mbunge wa tano wa eneo bunge la Mukurweini . Kama mbunge alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu fedha ,biashara ,utalii na mipango kabla ya uteuzi wake kama waziri chini ya utawala wa rais mstaafu Mwaki Kibaki . Kagwe baadaye alichaguliwa kuwa seneta wa kwanza wa Nyeri . Katika bunge la 11 alikuwa mwenyekiti wa kamati ya senate kuhusu ICT na kuhudumu kama mwanachama wa kamati ya senate kuhusu fedha na bajeti .Amewahi pia kuwa mwenyekiti wa kamati ya senate kuhusu Elimu .
Alipokuwa waziri , aliongoza ujenzi wa mfumo maalum wa Kebo ya mtandao wa East African Marine System – mradi mkubwa sana na wa kipekee katika kanda ya afrika mashariki . Kagwe ndiy aliyefadhili mswada wa usalama wa mtandaoni na ulinzi wad eta katika senate .Mwaka jana aliteuliwa na waziri wa kawi Charles Keter kuhudumu katika tume ya uthibiti wa kawi na Petroli (EPRA).
Mwingine atakayejiunga na baraza la mawaziri la rais Kenyatta ni Betty Maina ambaye amekuwa akihudumu kama katibu wa kudumu wa wizara ya Mazingira na Misitu . Ameteuliwa kuwa waziri mpya wa Viwanda ,biashara na ustawi wa kibiashara . Maina pia amwahi kuhudumu kama katibu w akudumu wa katika idara ya uwekezaji na viwanda katika wizara ya viwanda na vyama vya ushirika . Aliwahi kuhudumu kama afisa mkuu mtendaji wa muungano wa watengenezaji wa bidhaa (KAM). Awali aliwahi kuhudumu katika nydhifa mbali mbali katika Taasisi ya masuala ya kiuchumi ,Kituo cha kimatiafa cha Biashara za kibinafsi na katika taasisi ya Uongozi nchini Kenya .