Mwalimu wa kike kajitia kitanzi kaunti ya Kakamega

Mwalimu wa kike katika shule moja ya msingi eneo la navakholo kaunti ya Kakamega, amejitia kitanzi kwa kile kinachodaiwa kuwa ubishi wa ndoa baada ya mumewe kuoa mke wa pili katika kiji cha malaha.

"Hatujui ni nini ilitendeka inaweza walibishana na bwana yake, kwa sababu ya bibi wa pili, ugomvi ulianza wakati mume wake alioa bibi wa pili, na hakutuambia jambo lolote ama lilitendeka," Alieleza mwanafamilia mmoja.

Wanafamilia wamesema marehemu Aisha Anekeya hajawaambia lolote lilopelekea yeye kujitoa uhai.

"Kitu ili mbaya sana na jambo la kusikitisha ameacha watoto watatu wachanga sana wasichana wawili na mvulana kitinda mimba," Shemeji mmoja alisema.

Muungano wa walimu wa shule za upili katika kaunti ya Kakamega unaitaka serikali kupitia kwa wizara ya elimu kubadili mtindo wa kupeana vitabu kwa shule pasipo kuwahusisha walimu jambo linalopelekea utoaji wa vitabu aina moja

"si kuleta tu vitabu vya aina moja ama kuleta vitabu maradufu, wangoje idadi ya wanafunzi ni wangapi si kuleta tu vitabu, tunauliza idara hiyo kufanya kazi pamoja na walimu,"Alizungumza Wabuti.

Mwenyekiti wa KUPPET kaunti ya Kakamega Johnston Wabuti amesema ni makosa kwa serikali kutoa vitabu aina ile ile iliyotolewa mwaka jana badala ya kubadili vitabu na pia kuvitoa kulingana na uhaba.

KWINGINEKO: Nikuwa...

Kaunti ya Taita Taveta imeushtaki muungano wa wauguzi nchini KNUN na viongozi wa muungano huo katika tawi la Taita Taveta kwa kukaidi amri ya kusitisha mgomo unaoendelea.

 Kesi dhidi yao inatarajiwa  kuanza leo (Ijumaa) mbele ya jaji Farah Amin katika mahakama kuu ya Voi.

Yote tisa kumi nikuwa wauguzi hao wameendelea kushirikiana na msimamo wao kuwa hawatarejea kazini hadi pale matakwa yao yatakapotimizwa.

Lakini swali kuu ni je nani atakaye wahudumia wagonjwa licha ya wauguzi hao kutomaliza mgomo wao, na ni wangapi tayari wameumia katika hospitali hiyo.
Iwe mtoto, kijana mzee au mama anayetaka kujifungua nani atakaye wasaidia? Kabla sijatia kikomo matakwa ya wauguzi itatimizwa lini ili wagonjwa waweze kupewa huduma?