Mwanabiashara kuto jua uhusiano wa mkewe na mpwa wake

Janet waiyaki
Janet waiyaki
Mwanabiashara katika kaunti ya Nairobi hakujua uhusiano wowote wa mkewe na mpwa wake, George Kirubu jana aliweza kukumbusha mahakama ya Nairobi, vile alivyo pata habari za kifo za mke wake wa pili mwaka jana mei maeneo ya City park.

Alisema kuwa Janet Waiyaki, 41, alikuwa katika kampuni ya mpwa wake.

Pia aliweza kusema kuwa walikuwa na watoto watatu wakiwa na Janet ,na walikuwa na biashara pamoja inayoitwa Fay mobile.

Kirubi pia ana biashara ya mkahawa pia na duka la kuuza pombe eneo la Tom-Mboya Ronald Ngala. Mke wa kwanza wa Kirubi anaishi karibu na kituo cha polisi cha Pangani, na mke wake wa pili alikuwa anaishi katika eneo la Donholm.

Katika ndoa yao Kirubi na mkewe Janet wange tofautiana kwa mambo kadhaa lakini ni jambo la kawaida katika uhusiano.

"Katika ndoa watu huwa wanateteshana na pia kubishana na kisha kutatua shida zao, lakini nilikuwa  na mjali sana mke wangu." Alizungumza Kirubi.

Mwezi wa tano 20 mwaka jana Kirubi alitoka nyumbani kwake Pangani kisha kuelukea katika maeneo ya Donholm kwa mke wake wa pili.

Alipofika saa 9 asubuhi aliwapata watoto wake wakiwa na yaya. Aliweza kumpigia Janet simu ilhali hakupokea simu ya Kirubi.

Saa 10:00 asubuhi aliweza kupokea simu kutoka kwa binamu wake akimuuliza kama amepokea ripoti yeyote kisha akamjibu kuwa hamna ripoti ambayo amepokea.

Kuria hakumuelezea kinagaubaga kwanini aliweza kumpigia simu bali amwambia aende katika hospitali ya Avenue mahali mkewe alikuwa amepelekwa.

Kabla ya Kirubi kuenda aliweza kupokea simu ya pili kutoka kwa dadake marehemu kisha akamwambia kuwa Janet amefariki, ndipo aliweza kuchanganyikiwa afanye nini wala aseme nini.

Kirubi alienda kwa dadayake Janet ndiposa waweze kuenda hospitalini.

Janet alipigwa risasi na polisi wawili, alipokuwa katika gari ya mpwa wa Kirubi, Bernard Chege, 26, Chege alipata majeraha na amenakiliwa kama shahidi katika kesi hiyo.

Kirubi aliambia mahakama kuwa hajui kama wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na hajui kwanini walikuwa pamoja asubuhi ya kitendo hicho.

"Hii ni jambo la polisi kufanya uchunguzi,na ndio maana tuko hapa mahakamani," Hivyo ndivyo Kirubi alitoa ushahidi wake katika mahakama.

Katika mahakama Kirubi aliulizwa kama anamjua Chege hakuweza kujibu kwa maana mawazo yake hayakuwa katika kesi hiyo, bali alikuwa ana mkazia macho jaji Stella Mutuku.

Ilimbidi jaji huyo kumuita Kirubi na kumuuliza kama ako sawa. "Uko sawa," Mutuku aliuliza.

"Ndio niko sawa," Alijibu Kirubi. Aliendelea kupeana ushahidi wake akiwa amesimama. "Wakati huo wa kitendo hicho mke wangu alikuwa na huyo kijana wa ndugu yangu huko City park," Alieleza Kirubi.

Alisimama kwa muda wa dakika 10 akapeana ushaidi wake ndipo alisikia amechoka na kuomba koti aweze kuketi apeane ushahidi akiwa ameketi.

Mmoja wa wakili wa ulinzi aliweza kuomba mahakama aweze kupeana ushahidi ama akomeshwe kutoa ushaidi wake kwa maana alikuwa anasema kuwa shahidi huyo alikuwa amelewa.

Lakini wakili Ham Lagat alisema kuwa kusikizwa kwa kesi hiyo kuendelee.