Mwanadada asimulia alivyomlipia karo mumewe baadaye akamgeuka

photo-1505150099521-fde7970bcc3a
photo-1505150099521-fde7970bcc3a
Mwanadada amefunguka A-Z jinsi alivyopiga hasara ya kuingia mfukoni kutoa kitita kikubwa cha hela ili kusomesha mwanamume mpenzi wake.

Mwanadada huyu alipiga simu katika kituo cha utangazaji chini na kusimulia alivyohangaikia mwanamume wake na baadaye akakosa kupata usaidizi wake.

"Tulipokutana na mume wangu sote tulikuwa na vyeti vya diploma na tulifanya kazi sehemu moja. Kulitokea nafasi yake kuendeleza masomo na nikatoa pesa asome chuo kikuu apate digrii..."

Kumbuka kuwa katika mahusiano, watu huangaika sana ili wenzao wanufaike.

Sio mara ya kwanza kisa kam hiki kufanyika katika wanandoa.

Alichapa kazi kwa bidii ili mume wake amalize chuo kikuu.

"Nilikuwa namlipia karo yake yote. Mwanzo nilimpa kitita cha 240,000 ili alipe karo na pahali pa kuishi. Alipomaliza masomo alikuja nyumbani na akawa anataka kazi inayolipa mshahara mzuri zaidi..."

Mwanadada huyu hakusita kutoa pesa ili kumfadhili kabla apate kazi hiyo.

Kulikuwa na nafasi ya kazi ila hangeweza kuipata kwa urahisi kwa hivyo akaniuliza nimsaidie. Kazi yake ya awali alikuwa anapata 30,000 kwa mwezi. Baada ya kumhangaikia akapata kazi ya 170,000..."

 Baada ya kupata kazi mume wake aljawa na kiburi,

"Wakati ukafika wangu niende shuleni sasa niendeleze masomo kama yeye. Hakunisaidia kwa lolote na wala hakuja katika hafla yangu ya kufuzu chuo kikuu..."

Japo alimsamehe mume wake, bado anahisi usaliti mkubwa ulifanyika.

Je, unaweza kumsomesha mpenzi wako?