Mwanafunzi afariki kwenye dimbwi la maji

Hali ya simanzi imetanda katika shule ya msingi ya St Joseph mjini Webuye baada ya mwanafunzi mmoja kufariki baada ya kuzama alipokuwa akiogelea na wenzake.

Mwanafunzi huyo Hagai Matei alikuwa na wenzake katika mashindano ya kaunti ya kambi ya wanascout katika taasisi ya mafunzo ya Matili eneo bunge la kimilili kabla ya kuondoka na kuenda kwenye kidimbwi la maji kuogelea kabla ya mkasa huo.

Mwili wa mwanafunzi huyo ulitolewa kwenye kidimbwi hicho na wasamaria wema na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kaunti ya Webuye.

Kwingineko ni kwamba

Familia moja kijiji cha shibuye eneo bunge la shinyalu kaunti ya kakamega imepata msiba mara mbili baada yam zee wa boma kufariki pindi tu baada ya kupata habari za kifo cha bintiye aliyekuwa emeenda hospitali kuu ya kakamega kujifungua

 Mzee Julius atsango wa miaka 51 alipatwa na mshtuko wa moyo alipoata habari ya kfo cha bintiye Brenda shimekha wa miaka kumi na minane.

Pia

Polisi wa kakamega wamezindua kampein ya kutafuta taarifa kuhusu vijana ambao wametoweka makwao kwa muda bila kujulikana waliko kubaini iwapo wanajihusisha na visa vya ugaidi

Kamishona wa kaunti ya kakamega abdulrizak jaldesa ameyafichua hayo kwenye kongamano la kuangazia visa vya ugaidi mjini kakamega na kuwataka wazazi na jamaa kushirikiana na serikali kufanikisha juhudi za kuwaanika wale wanaohusika na ugaidi.