Mwanamke afariki Nairobi akiwa chumba cha kulala alichokodi na shemejiye

KNH
KNH
Mwanamke mmoja amefariki hapa Nairobi baada ya yeye na shemejiye wa kiume kalala usiku kucha katika chumba cha kukodi.

Kulingana na taarifa ya polisi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 42 ambaye alikuwa mkaazi wa mtaa wa Mwiki-Kasarani anasemekana kutangazwa kufariki alipofikishwa katika hospitali kuu ya Kenyatta asubuhi siku ya Alhamisi.

Ripoti ya polisi yaonyesha kwamba shemijiye mwenye umri wa miaka 45 kutoka kaunti ya Taita Taveta alikuwa amesafiri kutoka Malindi kuja Nairobi siku ya Jumatano.

Alipofika Nairobi siku hiyo mwendo wa saa moja unusu jioni, alikutana na mwanamke huyo (marehemu) ambaye alikuwa mke wa kakake na wakakodisha chumba cha kulala katika Hoteli ya Greenland iliyoko barabara ya Dubois ambapo walilala hadi asubuhi.

Kulingana na  ripoti iliyoandikishwa katika kituo cha polisi cha Central siku ya Alhamisi Asubuhi, mwanamke huyo alipata matatizo ya kiafya na kuanza kukohoa na kutapika.

Mwanamume huyo kisha alichukuwa teksi na kumkimbiza katika, Hospitali ya Kenyatta ambapo alitangazwa kufariki alipowasili na kupiga ripoti kwa kituo cha polisi cha KNH kwa nambari ya OB14/24/9/2020

Mwili wake unahifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Kenyatta ukisubiri kufanyiwa upasuaji kubaini nini kilimuua huku maafisa wa DCI nao wakianzisha uchunguzi wao pia.

Soma habari zaidi hapa;