Mwanamke Dandora, ajifungulia nje ya hospitali kwa kukosa shilingi 20

sonko
sonko

Gavana Sonko aliwasimamisha nesi wawili kazi kwa mda mtaani Dandora kwa kumwacha mama aliyekuwa karibu kujifungua ajifungue mtoto wake nje ya hospitali kwa kukosa shillingi 20 ya usajili.

Mabinti hawa wawili walisimamishwa kazi kwani Sonko alipata ujumbe kuwa, kuna mwanamke aliyejifungua nje ya hospitali.

Papo hapo, Sonko alisema kuwa lazima utafiti wa hali ya juu ufanywe kubaini ukweli wa kilichodaiwa.

Vilevile, Sonko alisema kuwa anataka majibu kabla ya masaa ya biashara kufungwa na akazidi kusema kuwa, maisha lazima yaheshimiwe.

         “I want answers before close of business tomorrow. Human life must be respected,”

Nesi hawa hawatakuwa kazini hadi siku ambayo utafiti utafanywa vizuri na wajue ni nini kitakachofanyika baadae.

Mtendaji wa afya katika kaunti ya Nairobi, bwana Mohamed Dagane alisema kuwa lazima hatua ichukuliwe iwapo kinachosemekana ni ukweli.

Dagane alisema kuwa, mwanamke huyo alijifungua nje ya hospitali kwa sababu alikosa shilingi 20 ya kuwahonga nesi hao na akasema kuwa, kitu kama hicho hakiwezi kubaliwa.

Vilevile Dagane alisema kuwa, huduma zote za uzazi ni bure kabisa na kwa hivyo, hakuna mtu anayetakiwa kulipa pesa yotote.

"No one is supposed to be subjected to inhuman delivery experiences in or outside our health facilities," Aliongeza.

Je? Walichofanya nesi hawa ni ungwana?