Mwanamme Kamili? Jamaa akiri kuwa na bibi WATATU huku wawili kati yao wakilala pamoja naye katika kitanda kimoja!

Daktari mmoja wa Tanzania JJ Mwaka amefichua jinsi alivyowoa wanawake watatu . Amesema ameweza kuata raha za wake zake wote bila  matatizo na amefurahia sana  hali ya maisha yake.

Akizungumza katika  mahojiano na Clouds Media  akiwa na mke wake wa pili na wa  tatu  Mwaka amesema  tama ndio iliyomfanya kuoa wanawake wengi  Amesema alimuoa mke wake wa pili bila mke wake wa kwanza kujua  lakini akapata ugumu kuendelea kuficha na hivyo basi akamtambua mke wake wa pili kwa wa kwanza . Mke wake wa pili amesema alifahamu kwamba mume wake alikuwa na mke wa  kwanza lakini alikuwa na utulivu ili kufahamiana naye na baadaye wakazoaeana .

Mke wa pili amesema baadaye waligundua mume wao walikuwa na mwanamke wa tatu na wakadhani ni uhusiano ambao utapita lakini baadaye   wakakubali kwamba mume wao alikuwa keshaoa mke  wa tatu! .

" Wakati wa likizo tunapokutana kama familia ,mke mwenza aliniarifu kwamba uhusiano wa mume wetu na Yule mwanamke wa tatu umekuwa  wa kudumu .Tulienda katika nyumba yake kumtafuta lakini hatukumpata ,tukachukua picha za  mtoto wake na kuziweka katika status zetu za whatsapp ili kumjulisha mume wetu kwamba tumeigundua siri yake ‘. Amesema mke wake  wa pili .

Mume naye aliamua kuziweka picha za wake zake wote watatu katika instagram  ili kuzikabili picha za mke wake wa kwanza na wa pili  jambo ambalo lilileta mgogoro hata zaidi . Mke wa pili anasema walitengana kwa muda lakini akakubali kukutana na mke wa  tatu kwa sababu naye pia alipokelewa na  mke wa kwanza .