Mwanamume ahukumiwa miaka 5 baada ya kukamatwa na pembe za ndovu

Mwanaumme mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 5 au alipe faini ya shilingi milioni moja na mahakama ya Voi, baada ya kupatikana na hatia ya kuwa na kilo 13.7 za pembe za ndovu.

Hakimu Hellen Nderitu alimpata na hatia hiyo Clinton Warunga ambaye alikamatwa na maafisa wa KWS akijaribu kuuza pembe hizo Oktoba mwaka jana katika eneo la Zongwani huko Mgheno, Taita Taveta.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu Nderitu ameitaka jamii kulinda wanyamapori.