Mwanamume aliyepashwa tohara kwa lazima aomba usaidizi

razor
razor
Mwanamume wa miaka 39 kutoka kijiji cha Lumboka eneo bunge la Bumula huko Bungoma aliyepashwa tohara kwa lazima ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kupitia gavana Kenneth Lusaka kuingilia kati na kuipa familia yake vyakula.
Mwanamume huyo ambaye ni baba wa watoto watatu, mume  na ni mhudumu wa bodaboda amesemakwamba kutokana na kupasjwa tohara akiwa mtu mzima amekawia kupona na hawezi kufanya kazi ili aipe familia yae chakula kwa sasa.
Wakaazi wa eneo hilo wamedai kua kupashwa tohara kwa jamaa huyo ilikua bora kwani ni lazima kwa mwanamume wa jamii ya wabukusu kupashwa tohara ili aweze kuwa mtu mzima na kamili katika jamii.