Mwanariadha Abraham Kiptum apigwa marufuku ya miaka minne

Mmiliki wa rekodi ya mbio za marathon Abraham Kiptum amepigwa marufuku ya miaka nne juu ya ukiukaji wa sheria za dawa za kupasha misuli, Kitengo cha Ushirikiano cha riadha (AIU) kimetangaza.

AIU ambayo inasimamia maswala ya uadilifu katika riadha za kimataifa, ikiwemo kupasha misuli ilikuwa imemzuia mwanariadha huyu wa miaka 30 tarehe Aprili 26, kwa ukiukaji wa pasi ya mwanariadha (ABP).

Pasipoti hiyo hutumia vipimo vya damu kugundua uwezekano wa kupunguka kwa kupasha misuli kuliko kupima vipimo maalum.

Marufuku hiyo ya miaka minne inaanza tarehe hiyo na matokeo yake yote kurudi had mwezi wa Oktoba 13, 2018 pamoja na rekodi ya half marathon ya (dakika 58 na sekunde 18) aliyoseti mjini Valencia mwezi huo huo wa Oktoba imefutiliwa mbali.

Wakati wake ulikuwa sekunde tano bora kuliko rekodi ya awali iliyowekwa na Zersenay Tadese wa Eritrea huko Lisbon mnamo 2010.

Mkenya mwenzake, Geoffrey Kamworor alivunja rekodi ya ulimwengu ya half marathon kwa sekunde 17 huko Copenhagen mnamo Septemba.

Kenya inajulikana kwa mbio za masafa marefu lakini sifa hizo zimeharibika kutokana na kesi kadhaa kuhusu upashaji misuli miaka iliyopita.