Mwanasiasa asimulia uchungu alionao baada ya watu,48, wa familia kupatikana na corona

Gordon Ogola
Gordon Ogola
Huku Wakenya weni wakiamini iuwa janga la corrona ni mzaha, familia moja ya aliyekuwa spika wa bunge la Migori Gordon Ogola imejitokeza na kusema kuwa kusema kuwa virusi vya corona viko, hii ni baada ya jamaa,48 zake kupatikana na virusi hivyo huku mmoja akiangamizwa na virusi hivyo chini ya saa 24.

Mwendazke tayari alikuwa mfanyakazi wa wizara ya ugatuzi ambaye alistaafu, atazikwa nyumbani kwake  hii leo God Ngoche katika kaunti ya Migori.

Ogola alisema kuwa wanaamini kuwa mama yao wa miaka,80, ndiye aliambukizwa virusi hivyo kisha akawaambukiza wanawe,wafanyakazi wa shamba wajukuu wake na baadhi ya jamaa zake, mama yake Ogola yuko hospitalini katika kitengo cha ICU akipigania maisha yake.

Kama vile waziri Mutahi Kagwe tusichukulie ugonjwa huu kwa kawaida ama utatuzidia, ofu yangu kubwa ni kwa ajili ya familia yangu na kijiji changu kikipatikana na virusi hivyo na kisha kiweze kusha chote, tuombeeni." Ogola Alieleza.

Gordon alikuwa spika wa Migori kati ya mwaka wa 2013 na 2017.Kutka kwetu wanajambo tunawaombea afueni ya haraka na Mungu alaze roho ya ndugu yake mahali pema peponi.