Kisasi cha laana! Mwanaume atolewa faini ya shillingi,5000 kwa kumtusi mamake

Leo katika mahakama ya kaunti ya Makueni mwanaume mmoja ameona cha mtema kuni kwa kutolewa faini ya shillingi 5000 kwa kumdunisha mamake mzazi kwa matusi.

Mwanaume huyo aliamrishwa atoe faini ya shillingi elfu tano la si hivyo afungwe kifungo cha miezi mitatu.

Pius Mwangangi aliyefikishwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo George Sagero alikubali madai ya kumwambia mama yake Monicah Mwangangi lugha chafu na kumtusi mnamo Februari,6, mwaka huu.

Alitema maneno hayo alipokuwa nyumbani kwao Kiuani kaunti ndogo ya Kathonzweni kaunti ya Makueni.

Mashtaka iliambia mahakama kuwa mshtakiwa alimtusi mama yake kwa kumuuliza swali na kutomjibu nani alizuia shamba yake siku iliopita.

Inadaiwa kuwa Pius aliamka kisu iliofuatia na kuenda katika jiko la mamake na na kumuamrisha amawambie nani alikuwa na ujasiri wa kuzuia shamba lake.

Pius aliomba msamaha mbele ya mahakama na kujuta kufanya kitendo hicho.

Katika mahakama hiyo kuna wanaume wawili _ambao walikuwa kizuizini kwa madai kuwa walifanya uhalifu, walikana madai hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya,100,000 wanaume hao walifahamika kama  James Mwendwa na Stephen Ochieng.

Wawili hao walikamatwa Februari,3, katika mji wa Wote walipokuwa wamebeba vifaa vya madini yasiosafishwa na walishukiwa kuwa wameiba .

Kusikizwa kwa kesi yao kutaanza machi,3, mwaka huu.