Mwanaume auwawa, pesa zaibiwa baada ya kuuza ng'ombe

Maafisa wa polisi mjini Kabondo Kasipul wamewakamata watu watatu wanaokisiwa kuhusika na mauaji ya mwanaume wa miaka 32 kwa ajili ya shilingi 9,000.

Kulingana na tovuti la The Star, inakisiwa Okeyo Obange aliuwawa baada ya vijana kadhaa kumfuata hadi nyumbani kwake, Ang’eny village, wodi ya Kojwach. Mwili wake ulipatikana karibu na lango lao asubuhi ya Jumamosi. Nyumba yake ilikuwa imevunjwa.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Rachuonyo Subcounty, Oyugis.

Inasemekana washukiwa walimuibia kabla ya kumuua. Alikuwa ameuza ng'ombe wake katika soko la wanyama lililoko karibu na kwake siku ya Ijumaa.

Chifu wa eneo hilo, James Oindi alisema kuwa washukiwa ni baadhi ya watu ambao Obange alikuwa ameshtaki kwa kumvamia wakati aliuza ng'ombe wake wa kwanza majuma mawili yaliyopita.

Obange alikuwa amepiga mayowe akilalamika kuwa nyumba yake ilikuwa imevunja na watu wasiojulikana na kujaribu kumuibia. Alipata majeraha wakti wa tukio hilo.

Waliomshambulia walitoweka baada ya kujaribu kumnyonga, kabla ya kurudi Jumamosi, wakti huu wakitamatisha misheni yao. Oindi alisema walipiga ripoti kuhusu mauaji hayo na uchunguzi unaendelea.

"Washukiwa wanaokisiwa wamekamtawa," Alisema akiwaonya vijana kuhusu kujihusisha na uhalifu.

"Hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria vijana ambao wanataka kula jasho la wengine."

Siku ya jumapili, kamanda wa polisi, Charles Barasa alisema washukiwa wamefungiwa katika kituo cha polisi cha Oyugis. Bado wanawatafuta washukiwa wengine.