Mwanaume kumkatakata mke wake na kuchoma mwili wake

Mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Eldoret aliweza kumtia kitanzi mke wake na kisha kuchoma mwili wake na kuweka mwili huo katika tangi la maji.

Ni kisa cha kusitikisha ambacho kimekumba familia na wana kijiji wa kaunti hiyo, mauaji hayo yalitokea baada ya mgogoro wa kifamilia kati ya wawili hao.

OCPD wa kaunti ya Eldoret John Owuor alisema kuwa mwanaume huyo aliweza kukamatwa na polisi jumatatu baada ya kufanya kisa hicho.

Jirani mmoja aliweza kusema kuwa mwanamke huyo waliweza kuja na mwanaume huyo kutoka klabu kisha kuishi kama mume na mke.

Hawakutia kikomo kwa kisa huyo mmoja akiongea na vyombo vya habari alisema kuwa mwanamke huyo na mwanaume walikuwa na mgogoro na kupigana kwa muda wa sasa.

"Kuna wakati niliona wawili hao wakichapana hadharani katika barabara, ilimbidi mwanaume huyo  kuanza kumchapa mke wake,

"Alimchapa huku akimvuta nywele zake ,kisha niliweza kujiuliza wawili hao wataweza aje kuishi kama wapenzi kama wanachapana hivi," Alieleza jirani.

Mwili wa mwendazake uliweza kupelekwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha Moi (Moi teaching referral hospita morgue)

Mwingine aliweza ongezea na kusema kuwa..

"Alikuwa amemkata kichwa na mikono yake kabla ya kumchoma, ni kisa cha kuhuzunisha," Jirani alisema.

Mwanaume huyo aliweza enda kwa rafiki yake na kumuambia waweze kuenda nyumbani kwake, walipofika aliweza kumuambia kuwa amefanya makosa kubwa sana.

Alimuuliza kosa gani kisha kumuambia amemuuwa mke wake."Walikuwa wanakosana na kupigana lakini aliniambia leo imeshindikana kwa maana nimemuuwa mke wangu," Rafiki yake alisema.

Polisi walisema kuwa mwanaume huyo aliweza kutumia panga kumkatakata mke wake kwa vipande kisha kumrusha kwenye tangi iliyo katika nyumba yao.

Hivi ni visa mabavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara,ama sanasana mwanamke kutoweka na kisha kupatikana akiwa amefariki.

Ni jambo la kiunyama ambalo liliweza kumkumba mwanamke huyo kisha kuaga dunia papo hapo.