Mwili wa mwanamke mjamzito wapatikana Mwiki

Mwili wa mwanamke mjamzito wapatikana kando ya barabara Mwiki.

Polisi wanachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamke mjamzito ulipatikana umetupwa kando ya barabara huko Mwiki jijini Nairobi. Wanasema inaonekana kana kwamba mwanamke huyo alipigwa na kifaa butu kichwani. Mwili huo ulipatikana na wakaazi wa eneo hilo waliowaarifu polisi. Hakuna aliyekamatwa kufuatia kisa hicho na mwanamke huyo hajatambuliwa.

Afisa wa magereza apatikana na hatia ya mauaji.

Afisa mmoja wa zamani wa magereza amepatikana na hatia ya kumuua mwanafunzi na kisha kuutupa mwili wake umbali wa kilomita mbili.  Dismas Motongwa alimgonga kwa gari Maureen Wambui kwenye barabara ya Mombasa na kisha kuutupa mwili wake mtaani South C.

Ukaguzi wa ugonjwa wa Ebola unaendelea Busia na Malaba.

Ukaguzi wa ugonjwa wa Ebola bado unaendelea katika mipaka ya Busia na Malaba ili kuhakikisha kua hakuna aliye na dalili za ugonjwa huo anaingia nchini kutoka Uganda. Evelyn Walela kutoka kwa wizara ya afya anasema pia wameweka ishara katika maeneo ya umma ili kuhamasisha kuhusu ugonjwa huo.

Mfungwa aliyefariki Naivasha alipigwa hadi kufa.

Mfungwa aliyefariki wiki iliopita katika gereza la Naivasha alipigwa hadi kufa. Uchunguzi wa maiti ya Simon Gitahi mwenye umri wa miaka 36, umefichua kuwa alifariki kutokana na majeraha mgongoni mwake ambayo yalisababishwa na kifaa butu.

Moto waharibu mali ya klabu moja Kasarani.

Mali ya thamani isiyojulikana iliharibiwa katika kisa cha moto jana kwenye kalbu moja mtaani Kasarani, jijini Nairobi. Meneja wa klabu hio aliyekua kazini alijeruhiwa alipokua akijaribu kuuzima moto huo. Polisi wanashuku kua moto huo ulisababishwa na gesi aliyokua ikivuja.