Mahakama kuu imeamuru kwamba Naibu jaji mkuu Philomena Mwilu hatoshtakiwa kwani ushahidi wa DCI dhidi yake ulipatikana kwa njia inayokiuka sheria .
Jopo la majaji watano hivyo basi limefutilia mbali kesi ya uhalifu dhidi yake kutokana na jinsi ushahidi huo ulivyopatikana .
Majaji hata hivyo wamesema kulikuwa na msingi ufaao wa kisheria kumfungulia mashtaka .
Idara za DCI na DPP zilikuwa zimemkabaa koo Mwilu na kupendekeza mashtaka kadhaa dhidi yake ikiwemo kutumia vibaya maamlaka yake kutokana na malipo aliyopokea kutoka kwa Benki iliyofilisika ya Imperial .
Kesi hiyo ilizua tofauti kubwa kati ya idara hizo mbili na ile ya mahakama kwani mtazamo wa wanaomwunga Mwilu mkono ulikuwa wa kuonewa kwa ajili ya msimamo wake wakati wa kesi ya Kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2017 .