Namzidi mpenzi wangu kwa miaka 50- Askofu Gilbert Deya

pastor deya
pastor deya
Baada ya kurejea nchini, askofu na mhubiri mwenye utata Gilbert Deya aliyegonga vichwa vya habari na skendo ya watoto wa kimiujiza muda uliopita amesema kuwa ana mpenzi wake wa nne ambaye anamzidi kwa miaka 50.

Soma uhondo hapa:

Mhubiri huyu amekuwa katika mahusiano mengi huku akiweka rekodi ya kuachwa na wanawake watatu. Kuna mwanamke mmoja ambaye alimtema baada ya kushika ujauzito wa mwanamme mwingine.

Kasisi huyu alikuwa anasimulia yote haya katika mahojiano na Massawe Jappani katika kipindi maridhawa cha Bustani la Massawe kinachoruka kupitia masafa ya redio Jambo.

Deya alisimulia jinsi alivyofungwa jela ya Kamiti baadaye kuachiliwa kwa dhamana ya Milioni 10 pesa taslimu.

"Nilifanya uamuzi wangu nioe hapa Kenya. Ni jambo la busara kuwa na mke ili kujiepusha na tamaa za mwili. Hapa Kenya wanawake ni wengi kama njugu mpaka serikali haina tatizo ukiwa na wanawake 50." alisema Deya.

Pata hadithi nyingine hapa:

"Nipo kwenye mahusiano. Wanaume wana changamoto ya kuona wanawake wazuri. Na ata kama umeokoka, macho hayawezi kuokoka." alisema Deya

Deya aliachwa na bibi yake kwa sababu ambazo hakuzitaja na kusema kuwa aliheshimu uamuzi wake.

"Siwezi nikawa sina mwanamke.Ningetaka nimwoe kwa sababu ni mchanga tunaachana na pengo la miaka 50."

"Bibi yangu aliamua kuniacha na mimi nikaheshimu uamuzi wake. Nilivumilia kwa miaka 5 na kwa sababu ya tamaa ya mwili nikaita wazee wa kanisa nikawaeleza kuwa nitaoa. Mke wangu wa kitambo anajua pia."