''Napigania haki za wakenya wote,'' Jimmy Gait amsihi rais Uhuru

Mwanamziki wa nyimbo za injili Jimmy Gait, alifunguka na kusema kuwa anapigania haki za wakenya wote wa kupata ushauri bora wa daktari kwani alikuwa amepewa ushauri usikokuwa sawa na daktari wa humu nchini.

Alipoulizwa sababu yake ya kupigania haki hizi alisema,..

1. Mtu anafaa kuwa huru kuuliza maswali. 

Jimmy Gait alisema kuwa, ni haki ya kila mwananchi kuuliza maswali yoyote anapoongea na daktari kwani mtu anafaa kujua mbona anapewa dawa hizo anazopewa na maswali mengine zaidi.

2. Rais anafaa kukubali kila mtu apewe ripoti yake ya hospitali.

Jimmy Gait alisema kuwa, alipokuwa India, alipewa ripoti yake yote ya matibabu na hivyo basi, kuomba Rais akubali watu wawe wanapewa ripoti zao ili mtu ajue anaugua ugonjwa upi.

3. Bodi za ugonjwa zinafaa kupewa kazi  

Vilevile, jamaa huyu alisema kuwa, bodi za hospitali zinafaa kuwekwa tayari na kupewa mamlaka ya kuchunguza kama kazi hospitalini inafanywa vizuri. Aidha, bodi hizi zinafaa kuwa zinaangalia wasiofanya kazi vizuri na kuwapiga kalamu .

4. Daktari yeyote wa serikali hafai kupewa ruhusa ya kuwa na kliniki ya kibinafsi.

Jimmy Gait alisema kuwa, madaktari wanaofanya kazi kwa serikali wanafaa kuwachwa wafanye kazi kwa serikali na kama wanafanya kazi katika zahanati zao basi wabaki katika zahanati hizo.