Naseeb Jnr kakua ! Tanasha Donna aonyesha picha zake

naseeb
naseeb
Hakika Tanasha Donna ni mama mwenye furaha tele.

Mama huyu ameonyesha tabasamu aliyo nayo na kuchapisha picha ya mtoto wake jinsi anavyokua mkubwa.

https://www.instagram.com/p/B6FhS5vho2A/

Tanasha alibarikiwa mtoto akiwa na mpenzi wake Diamond Platnumz wiki chache nyuma.

Kawaida wa wapenzi kuwa na hamu ya kuona mtoto wao akikua vyema.

Babake mtoto (Diamond Platnumz) alifarijika sana moyoni na kutoa hakikisho kuwa atamuoa mrembo huyu.

Kwa kile kinachoonekana kuwa somo kutoka kwa wanandoa na sherehe nyingi zinazofanyika nchini humo, Simba ameamua kufanya harusi na Tanasha Donna.

"Naomba mwenyezi Mungu atubariki. Mungu akipenda mwaka ujao itakuwa zamu yangu. Karibu kila mtu ninayemfahamu hapa ameoa kwa hivyo sina sababu ya kusema sitaoa pia. Nina mwanamke mzuri ambaye amenipa mtoto mrembo na sikosi chochote kutoka kwake..." Alisema Diamond Platnumz.

Mondi alisema tamko hili katika sherehe za ndoa ya dadake Queen Darleen.

Haya yanajiri baada ya staa huyu kuchapisha video katika mtandao wa Insta akionyesha mapenzi ya dhati akiwa na mrembo Tanasha.

Mondi amekuwa katika shughuli za tamasha na kwa hivyo hawajakuwa karibu na mama mtoto kwa siku kadhaa.