'Natembea na leso' mwanaume asema baada ya kunyofolewa Kakamega

Mwanamume wa miaka thelathini kutoka eneo la navakholo kaunti ya Kakamega analilia haki kutoka kwa serikali baada ya kundi la watu kumvamia na kumnyofoa sehemu zake za siri kasha kutoweka

Alfred sifuna nyongesa amesema anaisha kwa machungu na hata kuachwa na mkewe kufuatia kitendo hicho ile hali waliomvamia ni watu kutoka eneo hilo na ado wanamtishia maisha.

Watu walinisalimia kwa njia, wakanichukuwa wakanibeba wakanishika shingo wakanikata siri, waka chukuwa shilingi zangu mianane hamsini, natembea na leso, sasa hata mtu akiniona anastuka ni huyu ametairishwa ama na sehemu zangu zilienda. Sasa sijui walipeleka wapi. 

bib yangu ametoroka, hata watot wanatembea huku wakiranda randa.