'Natumaini akiba yetu itatuwezesha,' Msanii wa bendi ya sauti sol Bien Azungumza

Janga la corona limeathiri kila mwanabiashara na mwananchi, kutoka kwa wasanii maarufu zaidi, msanii wa bendi ya Sauti sol Bien alisema kuwa amelazimika kuishi kwa mrahaba.

Akiwa kwenye mahojiano Bien alisema uwa virusi vya corona vimemuathiri sana kifedha.

"Kwa sasa natagemea mrahaba kwa aana nimeandikia watu wengi nyimbo,mapema mwaka jana nilienda Germany kufanya nyimbo nyingi huko

Na kazi hiyo na nyimbo hizo ndizo zimekuwa zikinisaidia wakati huu, pia mrahaba unaopewa sauti sol wanaptia wakati mgumu akiba zangu zimeenda sana kwa maana mimi kama msanii napaswa kuwekeza

Natumaini akiba zetu zitatuwezesha mpaka pale janga hili litaisha."Alizungumza Bien.

Alisema kuwa hili si jambo rahisi kwa maana alikuwa na miradi nyingi kama vile kulipa wafanyakazi wake mishahara.

"Tuna video vya Bensoul na Nviiri na lazima zifanywe ili zisikae na wapoteze mwelekeo pia tuna nyimbo zingine zetu ambao zinahitajika kufanywa bali zimeathirika." Alisema.

Bien aliuliza serikali kuangalia ushuru kwa wasanii kwa ajili ya janga hili la corona kwa maana limewaathiri sana